TZ UPENDO KWANZA: GREATINGS TO THE WORLDTZ UPENDO KWANZA IS A RUNNIN...: GREATINGS TO THE WORLD TZ UPENDO KWANZA IS A RUNNING PROJECT WORK WITH ALL PEOPLE WITH AIM ,SPIRIT, AND LOVE TO SPREAD LOVE AND KNOWLEDGE...
talent found in street ,youth of Tanzania ,art product all in here
Sunday, March 29, 2015
Saturday, January 31, 2015
Mzazi unazipokeaje changamoto za mtoto wa mtaani
Kutoka na changamoto hizo idadi ya watoto waishio katika mazingira magumu nchini wamekuwa wakiongezeka kila kukicha, huku vituo vya kuwahifadhi pia vikiongekezeka mfano wa maduka ya kuuzia vocha za simu
Mara nyingi wanawake katika mikusanyiko ya jumuia huulizana swali hili ikiwa ni moja ya mbinu ya kuhamasisha suala la ulinzi kwa mtoto yeyote, anayeishi karibu yako, mbali na undugu au ukaribu alionao kwako.Kauli hiyo inafaa kuungwa mkono kwa asilimia mia moja kutokana na changamoto zilizojitokeza miongoni mwa watoto nchini huku sababu zikitajwa kuwa ni kuongezeka kwa umaskini,ujinga na maradhi.
Kutoka na changamoto hizo idadi ya watoto waishio katika mazingira magumu nchini wamekuwa wakiongezeka kila kukicha, huku vituo vya kuwahifadhi pia vikiongekezeka mfano wa maduka ya kuuzia vocha za simu.
Takwimu zinaonyesha kuwa kuna vituo 102 vya kulelea watoto hao, huku kituo kimoja kikikadiriwa kulea watoto wasiopungua mia moja.
Msingi mzuri wa malezi unajengwa na wazazi au walezi wenye mapenzi ya dhati kwa mtoto.
Kitaaluma mazingira ya kulelea watoto kwenye vituo hivyo siyo sahihi katika kumjenga motto. Inaelezwa kuwa hali hiyo inatokana na mrundikano wa watoto katika vituo vya kulelea watoto.
Kwa mfano katika kituo kimoja chenye watoto zaidi ya mia moja, watoto wapo chini ya mlezi mmoja au wawili. Ni jambo ngumu kwa walezi hawa kuhakikisha wanawadhibiti na kuwasimamia watoto katika misingi ya malezi yaliyobora kwa wakati mmoja.
Si hivyo tu, hali hiyo pia inaweza kuwaweka walezi katika mazingira magumu. Wanaweza kushindwa kumchunguza kwa karibu kila mtoto juu ya tabia na mwenendo wake wakati wa ukuaji. Wakati mwingine, inawezekana hukata tamaa na kukosa uchungu kwa watoto hao kwa sababu wao ni walezi tu.
Kuna rafiki yangu aliwahi kutembelea kituo fulani cha kulelea watoto jijini Dar es Salaam kilichokuwa na watoto zaidi ya mia moja. Baada ya kufika pale kituoni anaeleza kuwa hali na maisha aliyokutana nayo ilikuwa ya kusikitisha.
“Watoto wanaishi mfano wa jela ndogo. Kama mzazi, lazima itakuumiza tu,unaweza kutamani uwachukue nyumbani kwako, inaumiza sana. Wanaonekana wanyonge, huzuni muda wote, hata kama watapata muda wa kucheza hali waliyonayo ni tofauti na waishio majumbani kwa wazazi wao,”alisema.
Uzoefu unaonyesha kwamba, asilimia kubwa ya watoto wanaokulia katika mazingira ya vituo hivyo hupatwa na madhara mbalimbali ya kisaokolojia.
Mtoto anayekulia katika mazingira hayo,mara nyingi huathiriwa na tatizo la kutokujiamini, anaweza kuishi maisha ya hofu wakati wote kutokana na msingi wa malezi aliyokutana nayo utotoni.
Wengine huathiriwa na hali ya upweke tu, hata kama atakutana na maisha mazuri. Wengine wanaweza kuathiriwa na utegemezi. Mfano; nimewahi kukutana na kijana mmoja, ambaye historia yake inaeleza kulelewa katika vituo hivyo.
Kijana huyo alifanikiwa kuoa na kupata ajira mahali fulani, lakini bado alikuwa akienda katika ofisi za ustawi wa jamii bila hofu akihitaji msaada. Huyo ni mmoja kati ya watoto walioathiriwa na hali utegemezi.
Mbali na udhaifu huo katika vituo, wanasaikolojia wanasema hali hiyo inaweza pia kujitokeza hata majumbani, ambapo baadhi ya wazazi huwajengea maisha ya aina hii watoto wao tangu wakiwa utotoni pengine bila wao kujua madhara hayo.
Mwonekano wa malezi ulionayo inawezekana ni bahati kutokana na mazingira mazuri ya malezi uliyokutana nayo. Siamini kama Watanzania wote hatuna mazingira mazuri ya kiuchumi kuishi na mtoto hata mmoja aliyepo katika vituo hivyo.
Sidhani kama leo unaweza kuwa na furaha ikiwa utabahatika kuonana na mtu mzima ndani ya jamii akiwa na udhaifu kama huo niliouelezea hapo juu.
Watanzania tuamue kwa pamoja na kuona tatizo la watoto hawa ni letu sote, inawezekana changamoto hii ikamgusa ndugu, jamaa au rafiki yako pasipo kujua .
Tusijipime kiuchumi katika ushiriki suala hili bali kila Mtanzania anapaswa kuguswa na kuchukua hatua ya kukabili changamoto ya watoto wa mitaani iliyokithiri
Tuesday, January 27, 2015
2015 here we come
we take this moments to thanks our colleagues ,sponsor and friends who dedicate their time ,energy ,products and others stuff that made us to reach were we are so far the kids are doing well in art and we also manage to provide them other necessary stuff that help them to move and make them health while they are on their daily activities we got a lot of plans aim and courage we are well prepared to for 2015 sponsors ,friends,colleagues must expect more and we still need your support ,advice we gonna make it together lets create the smile together now
Subscribe to:
Comments (Atom)
